HISTORIA ya Zuchu Kutoka Wasafi | UMRI, MIAKA | MUME | PICHA | MAISHA YAKE


HISTORIA ya Zuchu Kutoka Wasafi | UMRI, MIAKA | MUME | PICHA | MAISHA YAKE

Zuhura Kopa anafahamika zaidi kwa jina lake la kisanii Zuchu; amezaliwa Novemba 22, 1993 ni mwanamuziki wa Kitanzania, mtunzi wa nyimbo na msanii wa kurekodi. Amesainiwa chini ya lebo ya WCB Wasafi Records chini ya uongozi wa Diamond Platnumz. Zuchu alitambulishwa  Jumatano Aprili 8, 2020 na Diamond ambaye ni mkurugenzi wa lebo hiyo na kufanya idadi ya wasanii wa WCB kufikia sita.

Zuchu alijulikana zaidi kwa wimbo wake “Wana”, ambao ulimtambulisha katika ulimwengu wa muziki. Kuongezewa kwa Zuchu kunaleta idadi ya wasanii kwenye lebo ya WCB Wasafi kuwa sita ambao ni pamoja na RayvannyMbossoLavalavaQueen Darleen na Diamond Platnumz mwenyewe. Zuchu anatoka katika familia ya muziki na asili. Yeye ni binti wa mwanamuziki wa kike wa Taarab anayeheshimika Khadija Kopa

Zuchu alianza kuimba akiwa bado mdogo na baadaye alishirikiana na mama yake Khadija Kopa kwenye wimbo uitwao Mauzauza kutoka kwa EP yake ya kwanza inayoitwa “I am Zuchu”.

Zuchu ni mtoto wa Khadija Kopa mkongwe wa taarab mwenye heshima tele katika tasnia. Aidha, Zuchu aliwahi kushiriki shindano la Tecno Own The Stage nchini Nigeria takribani miaka mitano iliyopita. Nandy alikuwa mshindi wa pili katika shindano hilo ambapo Shapera wa Nigeria aliibuka Kidedea

Mpaka sasa zuchu ameshaachia EP yake inayoitwa Iam Zuchu pia nyimbo zingine zinazosumbua Afrika Mashariki. Pia Zuchu anaweka rekodi ya mwanamke wa pili kusajiliwa katika lebo ya WCB wasafi

Mwaka 2020 Zuchu alifanikiwa kushinda Tuzo ya Afrimma – Best Newcomer

Nyimbo zote za Msanii Zuchu Tangu ameingia Wasafi ziko hapa: Nyimbo za Zuchu


1 comment: